Moja ya stori ambayo nimeipata leo ni kumhusu Muigizaji wa tamthilia za watoto maarufu ya Teletubbies aliyekuwa akijulikana kama Tinky Winky kwa wapenda Katuni wengi wanamfahamu kwa jina hilo, ila jina lake halisi Simon Shelton Barnes amefariki dunia akiwa na miaka 52 baada ya kuzimia kutokana na tatizo la ‘hypothermia’ katika mitaa ya Liverpool,
Simon Shelton Barnes ameacha watoto watatu, alipitia mafunzo ya kucheza ‘ballet’ na ‘choreographer’ kabla ya kuanza kuigiza kama kikatuni cha zambarau (purple Teletubby ) ambaye alikuwa akibeba begi la kimaajabu ‘magic bag’ katika tamthilia hiyo iliyoanza tangu mwaka 1998 hadi 2001.
Rafiki yake aliyeigiza naye John Simmit aliyecheza kama Dipsy alitumia ukurasa wake wa twitter na kusema “Ninakumbuka nyakati nzuri tulizokuwa pamoja”.
What a week ! RIP Simon Shelton aka Tinky Winky : remembering the many good times. Rest easy pic.twitter.com/4uyJDBoJdO
— John Simmit (@JohnSimmit) January 22, 2018
Days on am still processing this ! RIP Cyrille ??⚽️ pic.twitter.com/SnPuTiLL8m
— John Simmit (@JohnSimmit) January 18, 2018
Wengine walikuwa ni Nikky Smedley aliyekuwa kama Laa Laa, na Pui Fan Lee kama Po.