Siku kama ya leo miaka 32 iliyopita alizaliwa Kelly Rowland ambaye aliwahi kuja Tanzania na kufika hadi Uwanja wa fisi.
Kelly alikuja kwa ajili ya kampeni ya Staying Alive Foundation ambapo alikuwa balozi wa MTV AIDS Awareness.
Leo pia ni siku ambayo hayati Nelson Mandela aliachiwa huru kutoka kwenye gereza baada ya kuwa mfungwa hadi 11 February 1990.
Unaambiwa akiwa anatoka kwenye gerezani vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali za dunia walizunguka kuihabarisha dunia kwa kilichokuwa kinaendelea.
Kama haujawai kusikia sehemu inaitwa Silicon Valley huko Marekani basi jua kwamba hili ni eneo ambalo makampuni makubwa ya teknolojia yameweka makao makuu yao huko.
Ndani ya eneo hilo utakutana na makao makuu ya Google,Facebook,eBay,Adobe,Apple,Yahoo,HP,Intel,Mozilla Foundation,Linkedln,Twitter na mengine mengi.