Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) Kampasi ya Kikuletwa ilioko Hai Mkoani Kilimanjaro kwa hatua nzuri ya ujenzi wa majengo matatu yaliyopo Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambayo yanatarajiwa kuwa kituo cha umahiri katika nishati jadidifu.
Pongezi hizo zimetolewa wilayani humo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo,Husna Sekiboko kwaniaba ya wabunge wa kamati hiyo walipotembelea kampasi hiyo ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo yanayotarajia kukamilika Januari 15,2024 .
Majengo hayo yanayogharimu dola za kimarekani 16,250,000.00 zilizotolewana Benki ya Dunia (WB) na yamegawanyika kwenye loti tatu ambazo ni mabweni ya wanafunzi,majengo ya kujifunza,kumbi ya mikutano ,maabara ,mgahawa na chumba cha umeme ikiwemo ujenzi wa mabwawa wa maji taka.