Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepokea msaada wa fedha kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 5 kwaajili ya kusupport mamlaka ya mapato katika kuongeza kipato nchini na kuongeza nguvu katika kuzuia mianya ya ukwepaji kodi kwa Watanzania.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema>> ‘Serikali ya Kifalme ya Norway imetoa msaada kwa Tanzania katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kwamba tunaweza kuzuia wanaokwepa kulipa kodi‘
‘Wizara ya fedha tunataka kuondoka kutoka katika bajeti ya utegemezi na kwenda katika bajeti ya kujitegemea, lakini hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji wa mapato‘
‘Kwahiyo tunaishukuru sana Serikali ya Norway kwa msaada huu na pia tunawaahidi tutazitumia vizuri katika kuimarisha mamlaka yetu ya mapato na kazi zake kwa ujumla ‘
Ulimiss kumcheki Huyu jamaa kaigilizia sauti za Jakaya Kikwete na Rais Magufuli, kampatia nani zaidi?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE