Mtoto wa marehemu Amir Athumani maarufu kama Mzee Majuto, Athuman Amir amemshukuru Rais John Magufuli kwa msaada aliowahi kuutoa kwa marehemu baba yake wakati anaumwa.
Pia Amir amezishukuru Kampuni zilizowahi kuingia mikataba na marehemu baba yake kukubali kutoa fedha kama sehemu ya makubaliano ambapo pia amekabidhiwa hundi ya fedha kutoka kwa Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr.Harryson Mwakyembe baada ya serikali kufatilia mikataba ya marehemu Majuto.