Ikiwa nchi mbalimbali duniani zimeanza kufanya utafiti wa kutengeneza magari yasiyotumia mafuta, Japan pia imeanza kufanya utafiti wa kutengeneza magari ya mbao ngumu.
Hili linategemewa kuanza kufanyiwa utekelezaji kuanzia miaka 10 ijayo ikiwa ni pamoja na tafiti kuhusu kutengeneza magari ya material ya plastic ambayo yatakuwa rafiki kwa joto na kuchukua nafasi ya magari ya metali.
Wataalamu wanaeleza kuwa lengo kubwa ni kupunguza uzito wa magari pamoja na athari za hewa chafu na kelele ambapo watafiti katika Chuo Kikuu cha Kyoto wameeleza kuwa mbao kwa karne nyingi imetumika kutengeneza meli, nyumba na mengineyo na hivyo gari hizo za mbao zitakua na ubora uleule kama magari ya metali lakini yatapungua uzito kwa asilimia 80.
Ulipitwa na hii? TEKNOLOJIA: Kifaa kilichovumbuliwa kununulia Gas kwa miamala ya simu