Muungano wa Sacred Union for the Nation (USN) umemteua Félix Tshisekedi kama mgombea wa uchaguzi wa urais wa Desemba 2023 kwa niaba ya muungano huo.
Muungano huu unaojumuiha vyama vya kisiasa ulitangaza jina hili wakati wa kongamano lake la kwanza, lililofanyika jijini Kinshasa siku ya Jumapili Oktoba 1, 2023.
Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanasema wamemchagua Félix Tshisekedi ili kumruhusu “kumalizia alichoanzisha” kama rais wa DRC.
Viongozi kadhaa wa kisiasa walishiriki katika kongamano hili, hasa Jean-Pierre Bemba kutoka chama cha MLC, Vital Kamerhe kutoka chama cha UNC, Bahati Lukwebo kutoka chama cha AFDC, Christophe Mboso, na Augustin Kabuya kutoka chama cha UDPS, wote wanachama mashuhuri wa Muungano wa wa Sacred Union for the Nation (USN).
Hata hivyo, wagombea wengine wa urais pia wanajiandaa kukabiliana na rais anayemaliza muda wake Félix Tshisekedi.
Miongoni mwao, wapinzani Martin Fayulu na Moïse Katumbi ambao tayari wametangaza nia yao ya kugombea katika uchaguzi ujao wa urais.
Rais wa Félix Tshisekedi ambaye hakuwepo katika kongamano hilo, aliwasili mjini Lubumbashi akiambatana na mkewe siku ya Jumapili.