Listi ya mastaa au watu maarufu wa Tanzania ambao wametangaza kujiingiza kwenye siasa imezidi kuongezeka ambapo leo boss wa kundi la TMK Wanaume Said Fella, ametangaza kwa mara ya kwanza nia yake ya kujiingiza katika siasa na kwa sasa amevaa Gwanda la kugombea nafasi ya uongozi kwenye serikali ya mtaa Kirungule kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika ukurasa wake wa Instagram (@mkubwafella) ameomba watu wake waungane nae kwenye hili pia ili aweze kuichukua hiyo nafasi kwa kuandika ‘Leo wadau naomba dua zenu nagombea serikali ya mtaa huku kwetu Kitungule na nipo na Mgombea mwenzangu ndio tunagombania hiki kiti apate yeye au nibebe mimi Inshaallah’
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook