Kitabu cha pili cha maisha ya kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, “Alex Ferguson: My Autobiography”, kilichoanza kuuzwa mwezi October 2013, na kuuza jumla ya nakala 115,000 katika wiki ya kwanza na kuweka rekodi ya kuwa kitabu kilichouza kopi nyingi kwa haraka zaidi katika historia ya vitabu vya story za maisha halisi.
Kitabu hicho Ferguson pia kilikuwa kitabu kilichouza kopi nyingi zaidi katika mwaka 2013, kikiuza kopi 803,084.
Mauzo ya jumla ya kitabu hicho kinachouzwa kwa paundi 25 yamefikia takribani kiasi cha paund million 10, ikimaanisha kwamba kocha huyo mscotland amepata kiasi cha paundi millioni 1 (zaidi ya Bilioni 2 za kitanzania) kutoka kwenye asilimia 10 anayolipwa muandikaji wa kitabu kutoka kwenye mauzo.
Ferguson alitoa kitabu chake cha kwanza cha “Managing My Life: My Autobiography” mwaka 2000.