Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes alisema anataka kusalia katika klabu hiyo ikiwa timu ya Ligi ya Premia inamtaka, huku kukiwa na ripoti zinazomhusisha kiungo huyo wa kati wa Ureno kuondoka Old Trafford baada ya msimu mbaya.
“Ikiwa watanitaka nitasalia,” mchezaji huyo wa miaka 29 aliambia Sky Sports.
Fernandes alijiunga na United akitokea Sporting Lisbon mwaka 2020 na amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake lakini amekuwa akihusishwa na kuhamia kwa wababe wa Ujerumani Bayern Munich na mabingwa wa Italia Inter Milan.
“Nitakuwa hapa hadi… nilisema klabu inahitaji kunihitaji,” Fernandes alisema.
“Ninahisi kuwa klabu inataka niwe sehemu ya siku zijazo, kwa hivyo, kama nilivyosema siku zote, sitaki kuwa mchezaji ambaye klabu haitaki kuwa naye.”
United wamepoteza mara 14 kwenye ligi msimu huu, kiwango chao kibaya zaidi tangu kuanza kwa Ligi Kuu. Lakini waliweka hai matumaini ya Ulaya Jumatano kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wao wa mwisho wa nyumbani.
Wako katika nafasi ya nane kwenye jedwali lakini wana pointi 57 sawa na Newcastle inayoshika nafasi ya saba.