Leo May 25, 2018 Nakusogezea stori kumhusu kijana Teunis Tenbrook raia wa Uholanzi amefukuzwa katika chuo kikuu cha Erasmus cha jijini Rotterdam cha nchini humo kwa sababu ya kunuka miguu sana.
Baadhi ya wafanyakazi wa maktaba ya chuo hicho wamesema kuwa wamekuwa wakipata shida sana kufanya kazi kwa sababu kijana huyo miguu yake inatoa harufu mbaya mno hadi wanashindwa kutimiza majukumu yao.
Hata hivyo mwanachuo huyo anayesomea shahada ya falsafa amekishtaki chuo hicho na kushinda kesi hiyo huku Jaji aliyesikiliza kesi akiamuru kuwa wafanyakazi wa chuo hicho inawabidi “wazibe pua zao ili wasinuse harufu hiyo”.
Aidha tatizo la kunuka miguu imeripoitwa kuwasumbua wanafunzi wengi vijana.
VIDEO: Hatimaye Rufaa ya watuhumiwa wa ugaidi kuanza kusikizwa