January 16, 2018 watuhumiwa 25 wa kesi ya Ugaidi Arusha walivua nguo Mahakamani kwa madai ya kuchelewa kwa upelelezi katika kesi zao.
Leo January 30, 2018 Watuhumiwa hao 25 wa kesi ya ugaidi Arusha wamehukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kitendo cha kugoma kufika Mahakamani kwa ajili ya kutajwa kwa kesi zao.
Uamuzi huo umefikiwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha na Hakimu Nestory Baro baada ya Wakili wa serikali Augustino Komba kuiomba Mahakama kuchukua hatua za kisheria kwa kitendo hicho cha kutofika Mahakamani nakusema ni kuidharau Mahakama.
BREAKING: NECTA WANATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
GOOD NEWS: PAMBA YA MWANZA ITAPATA SOKO INDONESIA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA