Leo February 26, 2019 nakuletea stori hii kutokea nchini Ujerumani ambapo Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Balozi Dr. Possi akizungumza na AyoTV amesema kwamba mpaka sasa hana taarifa zozote zinazomhusu Mtu anayedaiwa kuwa Mtanzania ambae taarifa zake zilisambaa mtandaoni zikidai kwamba ameamua kukatisha uhai wake kwa hiari kwa kuchomwa sindano na Madaktari kutokana na kusumbuliwa na saratani ya damu.
Balozi Possi amesema amejaribu kutafuta taarifa za Mtu huyo ambae mtandaoni amefahamika kama Lizy mtango ikiwemo kuzungumza na Kiongozi wa Jumuia ya Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani lakini Kiongozi huyo naye amedai kutokuwa na taarifa zozote zinazomhusu Mtu anayetambulika kama ‘Lizy Mtango’.
Hata hivyo Balozi Possi amedai kwamba Ubalozi wake kutokuwa na taarifa za ‘Lizy’ sio kigezo cha kuthibitisha kwamba tukio hilo halijatokea kwani sheria haimbani Mtanzania kuripoti kwenye Ubalozi katika nchi anayokwenda.
UKITAKA KUOA WAHEHE WAZEE WA KAMWENE YAFAHAMU HAYA, KIANZIA MIA MBILI