Baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuwa na mwenendo mzuri katika soka kwa miezi ya hivi karibuni kiasi cha kufikia hatua ya kutinga hatua ya fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2019 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, imefanikiwa pia kupanda katika viwango vipya vya FIFA.
Tanzania imefanikiwa kupanda katika viwango vipya vya soka duniani vilivyotangazwa April na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, viwango hivyo vya mwezi April vimeitangaza Tanzania kupanda kwa nafasi 6 kutoka nafasi ya 137 hadi nafasi ya 131.
Hata hivyo Tanzania imekuwa na utamaduni kwa kushindwa kusimamia kiwango chake na kujikuta ikipanda na kushuka mara kwa mara, June 2018 ilishuka kwa nafasi tatu ambapo kwa wakati huo ilikuwa ya 137 ikashuka hadi 140 kabla ya kupanda tena na kurudin 137 na sasa ndio imepanda hadi nafasi ya 131, kwa sasa majirani zao Uganda wapo nafasi ya 79 na Kenya wapo nafasi ya 108.
Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….