Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.
Trump na Kagame wamekutana mjini Davos Uswizi, January 26, 2018 katika mkutano wa viongozi na watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara Duniani.
Katika mkutano wake na Kagame, Trump hajaonyesha kujuta kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika, amesifia mkutano wake na Kagame kuwa ni “wa kufana sana”, na kusema nchi hizo mbili zina ushirikiano wa kibiashara “uhusiano mzuri sana.”
Trump amempongeza Kagame kwa kuwa Mwenyekiti wa AU “Ningependa kukupongeza, Rais Kagame, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa.. najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza. Tafadhali, fikisha salamu zangu.”-Rais Trump
Rais Kagame amesema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika “operesheni zake kote Duniani”, pamoja na masuala ya kiuchumi na biashara.
VIDEO: JPM AMPA WASTARA MILIONI 15, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA