Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi na kujeruhi inayomkabili, Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Malima na dereva wake, Ramadhan Mohammed hadi November 1,2017.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, kuwa kesi hiyo iliitishwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na tayari walikuwa na shahidi ambaye ni Mwita Joseph, lakini kutokana na asili ya kesi hiyo , aliyepaswa kutoa ushahidi ni Daktari Mchwe Mpaka kabla ya Joseph.
Katika hati ya mashtaka, Malima anadaiwa kuwa May 15, 2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia ofisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake halali ya kumkamata Ramadhani Mohammed Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.
Ulipitwa na hii? MAHAKAMANI! Aveva, Kaburu walivyofika Mahakamani leo Sept 18