Nchi nyingi duniani zinaathririwa na ongezeko la wakimbizi kutoka nchi za jirani zinazosumbuliwa na matatizo ya vita za mara kwa mara, njaa, magonjwa na sababu nyinginezo.
Kutokana na hili serikali ya Ujerumani leo March 28, 2018 imetangaza njia mpya ya kuwafanya wakimbizi walioko nchi humo kuamua wenyewe binafsi kurudi kwenye nchi zao.
Waziri wa Maendeleo nchini humo Gerd Müller amesema kuwa serikali yake itatumia hadi Dola Milioni 620 ambayo ni sawa na Shilingi Trilioni 1.4 za Kitanzania ili kusaidia fedha kwa ajili ya kazi na programu za mafunzo ya ufundi katika nchi za Nigeria, Tunisia na Afghanistan.
Hii ni kufanya raia wa nchi hizo ambao wanaishi nchini Ujerumani kuamua kurudi nchini kwao bila kushinikizwa.
Upelelezi umekamilika kesi ya Malinzi, fahamu ilichopanga Mahakama