Kwa mara ya kwanza kwenye rekodi duniani ni taarifa inayotokea nchini Marekani siku za hivi karibuni kwamba mwanaume mmoja ameweza kunyonyesha mtoto.
Inaelezwa kuwa hii ni kutokana na kufanyiwa upasuaji wa kujibadilisha jinsia ili aweze kufanya jambo hilo baada ya mpenzi wake aliyejifungua kusema hataki kumnyonyesha mtoto huyo kabla hata hajajifungua.
Madaktari wanaeleza kuwa miezi mitatu kabla ya mtoto kuzaliwa, mwanaume huyo alianza kufanyiwa ‘matibabu’ hayo kwa kunywa dawa za kukamua maziwa na jambo hilo limewezekana.
Alipewa dawa hizo sambamba na kuwekewa homoni za kike ambazo huanza kusisimua utengenezwaji wa maziwa na kuzuia utengenezwaji wa homoni za kiume.
Mwanaume huyu wa miaka 30 ambaye jina lake halijawekwa wazi alikwenda kufanyiwa matibabu hayo katika kituo cha Mount Sinai’s Center for Transgender Medicine and Surgery kilichopo New York.
Lowassa ametaka athibitishiwe kama hawatomnyima kura Mgombea wa CHADEMA
Polepole, Lukuvi na Musukuma kwenye kufunga Kampeni za CCM Siha