Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango leo December 2017, katika uwekaji wa jiwe na msingi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Takwimu Mjini Dodoma amemkabidhi Rais John Magufuli zawadi ya ramani ya Tanzania inayoonesha hali ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kimkoa.
Katika makabidhiano hayo, Dr Mpango ameeleza kuwa kwenye takwimu za utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) juu ya hali ya maambulizi ya VVU kwa watu wenye umri wa miaka 15-49 kimkoa kwa mwaka 2016-17.
Ameeleza kuwa kiwango cha maambukizi mapya bado kiko juu kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ikiongozwa na Njombe 11.6%, Iringa 11.2% na Mbeya 9.2%.
Mikoa yenye maambukizi ya kiwango cha chini ni Unguja 0%, Kaskazini Pemba 0%, Lindi 0.3%, Manyara 1.8% na Arusha 1.9%.
Mkurugenzi wa Halmashauri na Mhasibu wanashikiliwa na TAKUKURU kwa ubadhirifu