Ni stori kutoka +256 Uganda kwa President Yoweri Museveni ambapo Bunge la nchi hiyo limepitisha muswada wa kuondoa ukomo wa umri katika kugombea Urais ambao ulikuwa ni miaka 75.
Mabadiliko hayo ya Katiba yamepitishwa kwa kura 315 dhidi ya kura za upinzani 62 yanampa nafasi Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania kiti cha Urais kwa Muhula wa Sita.
Tofauti na hilo wabunge pia wamerudisha nyuma ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano na kwa matokeo hayo wabunge wa sasa wataendelea kushikilia nafasi zao hadi mwaka 2023.
Ahadi ya TANESCO kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara