Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi inayowakabili vigogo wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Mbali na Dk. Tenga, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.
Wakili Kishenyi amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Victoria Nongwa ana udhuru, hivyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Hata hivyo, wakili wa utetezi Alex Mgongolwa ameutaka upande wa Mashtaka utoe taarifa kuhusu ulipofikia upelelezi, ambapo wakili Kishenyi amedai kuwa jalada lipo kwa DPP kwa sababu ya upelelezi.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 19,2018.
Ilipofikia kesi ya BILIONI 8 inayomkabili Wakili maarufu Dk. Tenga
MAHAKAMANI: Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’