Habari kutoka Jamhuri ya Urusi leo February 19, 2017 ni kwamba wanawake watano wameuawa kwa kupigwa risasi na kijana wa miaka 22 wakiwa kanisani.
Inaripotiwa na viongozi wa nchini hiyo kuwa wanawake wengine watano, ikiwa ni pamoja na afisa wa polisi na walinzi wa taifa, walijeruhiwa katika tukio hilo, wawili kati yao wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya.
Inaelezwa kuwa shambulio hilo lilifanyika wakati watu hao wakitoka kwenye ibada ya jioni kwenye Mji wa Kizlyar.
Aliyehusika katika shambulio hilo pia alipigwa risasi na kuuawa katika eneo hilo. Baadaye alitambulika kwa jina Khalil Khalilov ambaye ni mwanachama wa Kikundi cha Kiislam (IS).
Mwanamitindo maarufu Nchini aliyealikwa Ikulu ya Uingereza
Wakurugenzi wa Kampuni Nne wafikishwa Mahakamani kisa Wafanyakazi wao