Leo February 14, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba yupo Mkoani Singida akifanya shughuli mbalimbali za Serikali na Chama ambapo amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kama chambo ya kisiasa katika majukwaa.
Dr. Mwigulu aliyasema hayo February 13, 2018 wakati wa kampeni za udiwani katika kata ya Mitunduluni. Amewataka waache kutumia matatizo ya ndugu yao kama mitaji ya kisiasa baadala yake waje na hoja za maana za kusaidia katika maendeleo ya nchi.
“Fuatilieni sana wanaongea hayo ya Lissu mjue kama ni Wanasingida, mmoja nilimwambia Lissu unayemsema mimi ni ndugu yangu, wanakuja kuwaambia hivo kama chambo ya kisiasa, angekuwa mtu anayetokea Singida angepongeza Serikali kwa kazi ilizofanya baada ya Lissu kushambuliwa,” -Dr. Mwigulu
KAMANDA MPINGA AMETAJA WALIOKAMATWA NA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI YA MILIONI 33, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA