Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule (Professor Jay) alifika katika Mkoa wa Mbeya kwa dhumuni la kumtembelea Mbunge Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) akiwa ameambatana na Mkewe Grace Haule alifika Mbeya February 6, 2018.
Leo February 7, 2018 ameenda katika Gereza la Ruanda Mbeya kwa ajili ya kuwaona Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga ambapo amekataliwa kuwaona na uongozi wa Gereza hilo.
Sugu na Masonga wanatuhumiwa kwa kutoa maneno ya fedheha kwa Rais na kesho February 8, 2018 watafikishwa Mahakamani kwa ajili ya muendelezo wa kesi hiyo.
BREAKING: CHADEMA wazungumzia Diwani aliyetekwa ‘MULEBA’ na mengine