Leo April 5, 2018 Mahakama ya rufaa nchini Brazil imeagiza aliekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva kuwa ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na mbili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika ufisadi.
Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.
Lula amekutwa na hatia kutokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ”Operation Car Wash’‘
Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani Euro laki 7.