Mkali wa masauti, Christian Bella amefunguka na kuweka wazi kuwa kwasasa yuko mbio kuachia single yake mpya iitwayo Nishike ambayo video ya single hiyo itatayarishwa Afrika Kusini.
Akizungumza na Ayo TV staa huyo alisema..’Natarajia kusafiri kwenda South Africa kushoot video ya ngoma yangu mpya inaitwa Nishike unajua tangu mwanzo sijaachia ngoma siku nyingi kwahiyo natakiwa niachia audio pamoja na video, lakini South Africa nitaenda na msanii wa Hip Hop Fid Q yeye atahusika kuniandikia Script ya video hiyo mpya kwa ana utaalamu sana’- Christian Bella
ULIIKOSA HII YA ALIKIBA, OMMY DIMPOZ NA WEMA SEPETU NDANI YA STAGE MOJA NA CHRISTIAN BELLA BSI ITAZAME HII VIDEO HAPA