Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) mwezi huu linatarajiwa kupiga kura ya kuamua kuifutia uanchama Israel au la kutokana na kutenda jinai kubwa dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Taarifa zaidi zinasema, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) litapiga kura katika mkutano wake ujao mjini Bangkok tarehe 17 mwezi huu kuhusu ombi la Shirikisho la Soka la Palestina la kuiondoa Israel katika uanachama wa FIFA.
Shirikisho la Soka la Palestina lilituma barua ya kutaka kupigwa kura kuhusu kuondolewa kwa utawala wa Israel kutoka katika jamii ya soka kutokana na kukiuka haki za binadamu na kufanya mauaji ya kimbari huko Gaza. Shirikisho la Soka la FIFA litapigia kura pendekezo hilo katika mkutano ujao wa shirikisho hilo huko Bangkok.
Katika taarifa iliyotolewa Machi mwaka huu na Shirikisho la Soka la Palestina lilitangaza kuwa wachezaji 99 wa Kipalestina wameuawa pamoja na “kubomolewa kwa vilabu vya soka” tangu kuanza kwa vita vya Gaza.