Uchaguzi wa Rais wa Shirikisho la soka duniani umepangwa kufanyika Februari mwakani na tayari kuna baadhi ya wanamichezo wamejitokeza kuwania naasi hiyo.
Wengine ni Rais wa shirikiso la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini na Chung Mong-Joon wa Korea Kusini wameonesha nia yao kuwania nafasi hiyo.
Mwanamfalme wa Jordan Ali Bin Al-Hussain ametangaza kuwa atasimama kuwania nafasi hiyo kuwa duniani ili kurithi nafasi ya Rais wa sasa anayestaafu Sepp Blatter.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni zake mwanamfalme huyo aliahidi kufanya mageuzi katika uongozi wa soka,kupambana na rushwa na kuimarisha soka la wanawake.
Mgombea huyo alipoteza ushindi mwezi Mei ambapo Sepp Blatter alishinda kabla ya kutangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Maafisa wa ngazi ya juu ya FIFA wanatuhumiwa kuhusika na rushwa na mamlaka za Marekani mapema mwaka huu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos