Uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka duniani unatarajiwa kufanyika Februari 26, 2016 na tayari viongozi mbalimbali wamejitokeza kuwania nafasi ya Urais iliyokuwa ikishikiliwa na Sepp Blatter.
Musa Bility raia wa Liberia ni mmoja wa wanachama waliojitokeza kuwania nafasi hiyo lakini jina lake limeondolewa kutoka kwenye kinyang’anyiro hicho kwa sababu za kimaadili.
Mpaka sasa Shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limeidhinisha wagombea watano tu huku Rais wa UEFA Michel Platini naye pia hajajumuishwa kwenye orodha hiyo ya wagombea.
Waliopitishwa kuwania nafasi hiyo ni Mwana wa mfalme Ali bin al-Hussein, Jerome Champagne, Gianni Infantino, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa na Tokyo Sexwale.
Fifa imesema haitazungumzia zaidi sababu za kutemwa kwa Bility, ambaye amepanga kupinga uamuzi huo katika mahakama ya kutatua mizozo ya michezo na imeamua kutotoa maelezo zaidi kuhusu sababu hizo kwa maslahi ya Bility.
Kwa sasa Bility ndiye rais wa chama cha soka Liberia.
Sepp Blatter kwa sasa amesimamishwa kazi na anachunguzwa kwa tuhuma za ufisadi na nafasi yake imezibwa na Issa Hayatou kutoka Cameroon.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE