Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa mrejesho wa mkutano wa 66 wa UNWTO-Kamisheni ya Afrika ambao umefanyika Nchini Mauritius kuanzia tarehe 26 hadi 28 Julai, 2023. Lengo la Mkutano huo lilikuwa ni kujadili masuala mbalimbali ya kukuza utalii Barani Afrika kupitia kauli mbiu “Kukuza Uwekezaji na Ushirikiano na Kutatua Changamoto zinazoikabili sekta ya Utalii duniani” (Rethinking Tourism for Africa: Promoting Investment and Partnerships: Addressing Global Challenges) pamoja na kufanya chaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi katika shirika hilo.
Tanzania imeshiriki mkutano huo na kuweza kupata mafanikio kwa kunyakua nafasi nafasi mbali mbali za juu za uongozi katika shirika hilo kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika katika mkutano huo ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushinda nafasi hizo katika shirika hilo tangu kujiunga na uanachama wa shirika hilo
Tanzania imeweza kushinda nafasi mbalimbali zikiwemo (i)Makamu wa Rais wa Mkutano Mkuu wa Shirika hilo, Katika nafasi hii Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa ataliwakilisha Bara la Afrika katika nafasi ya Makamu wa Rais kwanye Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO); kupitia nafasi hii tutatangaza vivutio vyetu vya utalii katika masoko mbalimbali ya utalii Duniani kupitia mikutano na matukio yanayoandaliwa na UNWTO.
Nafasi nyingine ni (ii) Mjumbe wa Baraza Kuu Tendaji Ia UNWTO.
Katika nafasi hii Tanzania kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii itakuwa sehemu ya nchi zinazofanya maamuzi ya juu ya kuendeleza sekta ya utalii katika Shirika Ia Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani. Aidha, Tanzania itatumia fursa hii katika kuvutia miradi ya maendeleo ya utalii nchini na Afrika kwa ujumla.
Nafasi ya Ujumbe wa Baraza Kuu Tendaji ilikuwa ikiwaniwa na nchi 13 za Bara la Afrika ambazo ni Tanzania, Ghana, Congo, Namibia, Seychelles, Nigeria. Ivory Coast, Tunisia, Algeria, Mauritius, Senegal na Rwanda ambapo Tanzania imeweza kushinda na kupitishwa na nchi za Afrika kuwa moja ya nchi 6 zitakazoiwakilisha Afrika katika Baraza hilo.
Baadhi ya nchi zinazounda Baraza hilo ni pamoja na Afrika ya Kusini, Morroco, Umoja wa Falme za Kiarabu, Hispania, Italia, Ufaransa na Japan. Vile vile, kupitia nafasi hizi Tanzania itapata fursa ya kuleta matukio mbalimbali nchini kama mikutano na mafunzo Yenayolenga kuitangaza na kukuza utalii nchini pamoja na kushirikiana na nchi zilizobobee katika utalii duniani kama Afrika Ya Kusini, Falme za Kiarabu, Hispania na Ufaransa.
Kupitia matukio hayo Tanzania itaweza kuvutia wawekezaji katika sekta ya utalii nchini.
Pamoja na kushinda chaguzi mbalimbali katika Mkutano huo, yapo mafanikio mengine ambayo Tanzania ilitajwa katika Mkutano huo.
Mafanikio hayo ni pamoja na,Tanzania kutajwa nchi ya Pill Afrika kwa kuwa na ongezeko kubwa la watalii katika robo ya kwanza ya mwaka 2023. Nchi ya kwanza ni Ethiopia na ya tatu ni Morroco.Tanzania kutajwa na UNWTO tena kuwa ya pili Afrika baada ya Morocco kuvutia miradi mingi ya uwekezaji kutoka nje katika sekta ya utalii.
Mafanikio haya yanatokana na Serikali ya awamu ya sita ya Mheshimiwa, Dkt, Samia Suluhu Hassan kuonesha nia ya dhati katika kukuza na kuendeleza sekta ya utaul nchini na sisi watendaji wake tutaendeleza ubunifu na kujituma kuhakikisha utalii wetu unasonga mbele.