Timu ya taifa ya Mali ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano ya AFCON U-17, baada ya suluhu yao ya kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania leo May 18 2017 wamerudi uwanji kucheza dhidi ya Niger baada ya mchezo wa Tanzania na Angolakumalizika.
Mali ambao ndio Mabingwa watetezi wameingia katika uwanja wa Stade de Amitiekutafuta ushindi ili wajiweke pazuri katika mbio za kutetea taji lao na kupata nafasi ya timu nne zitakazofuzu nusu fainali kucheza michuano ya Kombe la dunia
baadae mwaka huu nchini India.
Mchezo huo wa pili wa Kundi B kati ya Mali dhidi ya Niger umemalizika kwa Mabingwa watetezi Mali kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ambayo yamefungwa na nahodha wao Mohamed Camara na Hadji Drame wakati Niger wameambulia
goli moja lililofungwa na Habibou Sofiane.
Ushindi huo wa Mali unawafanya kuwa sawa kwa point na Tanzania na kuwa sawa kwa kila kitu kwa maana ya magoli ya kufunga na kufungwa, Tanzania wana point nne wakifunga magoli mawili na kuruhusu moja sawa na Mali wakati Mali na Angola na wenye wakisalia na point moja wakifanana pia kwa kila kitu, Tanzania sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa mwisho dhidi ya Niger.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera