Baada ya kusota rumande kwa zaidi ya wiki moja, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamepewa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Dhamana imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama ya Kisutu kuiskiliza kesi hiyo.
Hata hivyo washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa ambayo ni kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya Ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.
Shtaka lililokuwa likiwakabili awali la kula njama limeondolewa kwenye hati hiyo ya mashtaka. Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana ambapo waliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Wakili Kimaro alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na washtakiwa watasomewa maelezo ya awali January 17, 2018.
SIKU YA II: Kesi ya M/kiti wa zamani wa CCM Ramadhan Madabida