Leo February 18, 2018 Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema uchunguzi wa tukio la kupigwa risasi kwa Mwanafunzi wa NIT utafanyika haraka iwekezanavyo kwa weledi na utaalamu ili haki itendeke.
“Tutafanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo, Serikali tunasikitishwa na kifo cha mwanafunzi Huyu, pia na majeruhi ya raia na askari Polisi wawili,” -Masauni.
Amesema Serikali haiwezi kuyaacha matukio haya yapite kama yalivyo, hivyo imeyachukulia kwa uzito unaostahili.
Maagizo ya Rais Magufuli kwa Vyombo vya Dola kwa Waliosababisha Akwilina Kupigwa Risasi