Watu saba wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kuiba mabunda manne ya nyaya za umeme zenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 100 mali ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Washtakiwa hao ni Mbatia Mhando 35, Abdallah Tambwambwa 39, Willy Mgimbuzi 32, Francis Nchimbi 50, Ally Mohammed 42, Hassan Haji 29, na Misana Selestine 27.
Wakili wa serikali, Herieth Loda amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa December 16, 2017 maeneo ya Tabata Kinyerezi DSM washtakiwa waliiba mabunda manne ya nyaya za umeme zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Pia Wakili Lopa amedai kuwa katika kipindi hicho kwa vitendo vyao washtakiwa hao kwa makusudi walisababisha hasara ya Tsh Milioni 116,872,813 mali ya TANESCO.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika ambapo washtakiwa wamerudishwa rumande, huku wakishauriwa kuomba dhamana Mahakama Kuu. Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi February 7, 2018.
BREAKING: Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Butiama
Jeshi la Polisi limetaja mambo ya kuzingatia kuelekea uchaguzi mdogo Kinondoni