Imekua kawaida matajiri wakubwa duniani na wajasiriamali kujulikana kutokana na jitihada zao binafsi tofauti na hapo zamani ambapo kwa asilimia kubwa utajiri ulipatikana kwa kurithi kutoka kwa wazazi. Jambo ambalo halijabadilika mpaka sasa katika baadhi ya nchi
Florence Marekani ni moja kati ya miji ambayo majina ya matajiri wake ni yale yale yaliyokuwepo tangu mwaka 1427 ambapo ni zaidi ya miaka 600 sasa.
Watafiti wa uchumi wamegundua kuwa majina ya familia zilizoingia katika list ya matajiri wakubwa mjini hapo hayajabadilika kwa takribani miaka 600 sasa. Wachumi Guglielmo Barone na Sauro Mocetti wamegundua kwamba zaidi ya majina 900 ya familia zilizokuwa na utajiri mkubwa hayajabadilika tangu mwaka 1427 utafiti uliofanyika mwaka 2011.
Hata hivyo rekodi za malipo ya kodi mjini hapo zinathibitisha juu ya kutokubadilika kwa majina ya matajiri katika mji huo miaka nenda rudi. Biashara zilizoanzishwa na wazazi wao zimeendelezwa na kuwa kubwa zaidi hali ambayo inasababisha utajiri kuongezeka. Kila aliyeweza kumiliki mali miaka 600 iliyopita aliziacha mali zake katika usimamizi makini.
ILIKUPITA HII YA MBUGE KANGI LUGOLA KUTOKUBALIANA NA WABUNGE KUKATWA KODI ‘MNATAKA TURUDI MTAANI MTUCHEKE’