Wakati Tanzania tukisubiri kukamilika kwa Flyover inayojengwa TAZARA mwaka 2018, zipo nchi mbalimbali duniani ambazo zimefanikiwa katika barabara za juu.
Leo April 12, 2017 nimekutana na hii ya list ya flyover 5 kali zaidi kuwahi kujengwa duniani.
1: Judge Harry, Marekani
Flyover hii imejengwa jijini Los Angeles, Marekani ambapo unaambiwa ina urefu wa zaidi ya futi 130 kutoka ardhini. Ilijengwa mwaka 1993 na ina uwezo wa kupitisha magari mazito ya mizigo.
2: Spaghetti Junction, Uingereza
Ilijengwa mwaka 1965 na kujipatia umaarufu mkubwa duniani kwa namna ilivyojengwa. Ilipewa jina la Spaghetti kutokana na namna barabara zilivyojinyonga.
3: Binhai, China
Flyover hii ilijengwa mwaka 2001 ikiwa na urefu wa kilometa 53 ambapo inaunganisha miji mbalimbali nchini humo.
4: High Five, Marekani
High Five ilijengwa mwaka 2001 na inapatikana katika mji wa Dallas, Marekani ambapo inayaunganisha zaidi ya madaraja matano. Iligharimu zaidi ya Dollar 261 million.
5: The Circle, Marekani
Ujenzi wake ulikamilika December 2016 na inapatikana katika mji wa Chicago, Marekani. The Circle ina uwezo wa kupitisha magari yenye uzito mkubwa na iligharimu zaidi ya Dollar 250 million.
VIDEO: Ulikosa kumuona Rais Magufuli akizindua mradi wa ujenzi wa intercange Ubungo, Dar es Salaam? Bonyeza play hapo chini kuitazama.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millarday