Kama umeweka vitu vyako vingi vingine vya siri zako kabisa kwenye kitu kama memory card, flashdisk na external hard disk, ikatokea bahati mbaya kifaa hicho kikapotea ni lazima utachanganyikiwa kutokana na kupoteza kitu chako chenye vitu muhimu!
Kampuni ya Toshiba na Corsair wametoa flash disks zenye keypad, halafu kingine ni kwamba hii itakuwezesha kuweka password katika flash yako, hakuna mtu mwingine ataweza kuifungua na kuona kilichomo ndani zaidi ya wewe mwenyewe unaezijua namba za siri.
Iwapo mtu akijaribu kuingiza password zaidi ya mara kumi flash hiyo itafuta data zote zilizomo, hii itakusaidia kama kuna vitu vya siri basi hakuna atakayeweza kuvitoa.
Toshiba imesema itaingiza sokoni flash hizo ambazo zitakuwa na ukubwa wa kuanzia 4GB, 8GB, 16GB na 32GB, upande wa bei pia ni kuanzia dola95 (laki 170,000/= Tshs) hadi dola 200 (360,000= Tshs)
Unadhani hii itasaidia kweli kuweka ulinzi wa vitu vyako kama picha na vitu vingine kuvuja? Kama una chochote unaweza kuniandikia mtu wangu.