BBC imeripoti kwamba watu 12 wamefariki kwenye nchi ya Indonesia kutokana na foleni ya magari iliyosababisha mamilioni ya watu kukwama barabarani siku kadhaa.
Wengi walifariki kutokana na kukosa maji mwilini na uchovu ambapo wengi waliokuwa wakisafiri kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, walikusanyika katika makutano ya barabara kisiwa cha Java.
Na hapo ndipo msongamano mkubwa wa magari ulipotokea ambapo mamlaka zimesema vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha siku tatu wengi waliofariki ni wazee ambao walikwama ndani ya magari chini ya joto kali na mtoto mmoja mchanga alifariki kutokana na kinachodhaniwa kuwa ni kupumua hewa chafu iliyojaa moshi wa magari.
ULIIKOSA YA MABASI YA KISASA KWA MARA YA KWANZA DAR? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI