Kwenye moja ya ahadi za Dr. John Pombe Magufuli wakati akiwa kwenye kampeni ya kugombea Urais wa kuiongoza Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ilikua ni kujenga barabara za juu kwenye jiji la Dar es salaam ili kusaidia kupunguza foleni.
Rais Magufuli aliingia kwenye headlines za moto ndani ya saa 24 tu baada ya kuapishwa kwa kuanza kufanya ziara za kushtukiza kwenye taasisi za serikali kama Wizara ya fedha pamoja na hospitali ya taifa Muhimbili akionyesha kwamba kazi ndio imeanza, na sasa anazimiliki headlines kwenye barabara za juu.
Yafuatayo ni mambo matano ambayo yatakupa uhakika kwamba barabara za juu Dar es salaam zinanukia na mradi wake umeanza kufanyiwa kazi, ungana na Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Injinia Felchesmi Mramba kwenye kauli zake baada ya TANESCO kuambiwa isogeze mitambo yake kupisha ujenzi wa hizo barabara.
1 – ‘Ni kweli ipo kazi kubwa inayofanywa na serikali kupanua barabara na kuweka barabara za juu katika maeneo mawili ambayo ni TAZARA na Ubungo.
2 – Kwenye maeneo yote mawili miundombinu ya umeme ya TANESCO ipo na hasa eneo la Ubungo ambako kuna laini kubwa, kwa TAZARA tayari tulishahamisha laini zetu na kupisha eneo la upanuzi wa hizo barabara za juu na sasa zinaweza kujengwa bila tatizo.
3 – Kwa Ubungo kuna kazi kubwa zaidi kuliko TAZARA kwa sababu ya kuhamisha laini kubwa ya KV 132, kazi ya kuihamisha itaanza mwezi wa kwanza mwaka 2016 na itaweza kuchukua miezi kama mitatu mpaka sisi kumaliza kuiondoa.
4 – Laini kubwa inayotoa umeme kutoka Ubungo kwenda kituo kikubwa cha katikati mjini cha Ilala ndio inayotakiwa kunyanyuliwa juu sana kwahiyo tutajenga minara mipya mirefu zaidi ambayo itakwenda juu zaidi.
5 – Kazi ya TAZARA imefanywa na Mainjinia wa Kitanzania ila hii ya Ubungo ambayo ni kazi kubwa itafanywa na Mainjinia wa Kijapan.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.