Baada ya Pambano la Floyd Mayweather VS Andre Berto ambalo walipigana usiku wa kuamkia September 13 2015, Mayweather aliongea kauli hii >>> ‘Nimekamilisha kila kitu, nimefanya kila kitu kwenye mchezo wangu… Umri wangu unakaribia miaka 40, hakuna nilichobakiza kwenye Ulimwengu wa Ngumi, nahitaji kutumia muda mwingi zaidi na familia yangu‘>> hii ilikuwa ni uthibitisho wake kwamba yeye na masuala ya Boxing ndio yamefikia mwisho !!
Nje ya Ulingo stori ziko nyingi sana, japo watu wengi hawakuvutiwa na Pambalo kati ya Mayweather na Berto kutokana na kupishana kwa Rekodi zao, kuna list ambayo imepangwa na Wachambuzi wa mambo wanasema Floyd Mayweather hawezi kuishia kuandika Rekodi ya kushinda mapambano 49, wanasema lazima jamaa ataongeza pambano moja ambalo akishinda atakuwa ameandika Rekodi ya kucheza Mapambano 50 na kushinda yote ndani ya kipindi cha miaka 19 ambayo amekuwa Bondia.
Floyd ‘Money’ Mayweather anarudi Ulingoni? swali jingine ni kwamba anarudi na nani kati ya hawa wenye Rekodi za nguvu kabisa? Atafanikiwa kuandika Rekodi ya Ushindi kwenye Pambano la 50?
Majibu yatapatikana soon, kama pambano hili likithibitishwa basi story huenda ikawa kubwa pamoja na promo ya nguvu ambayo inaweza kufananishwa na Rekodi ya mauzo makubwa yaliyofanyika kabla ya Pambano la May 02 2015, Floyd Mayweather VS Manny Pacquiao..
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE