Ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita imekuwa ikiripotiwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari huku ikisubiriwa kutolewa majibu na Mahakama Kuu Mwanza kuhusu hatma ya zuio hilo.
Leo maamuzi ya Mahakama Kuu Mwanza yametoka na majibu kwamba wanaCHADEMA na viongozi wao wamepata kibali cha Mahakama hiyo kuendelea na shughuli za kuaga pamoja na mazishi ya kiongozi huyo.
#Breaking Familia ya Marehemu Mawazo wa CHADEMA Geita imeshinda kesi iliyofunguliwa kupinga mwili wa marehemu kuagiwa Mwanza.
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Nje ya Mahakama Kuu Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe alipata dakika chache kuongea na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakisubiri kusikia maamuzi ya Mahakama >>>> “Ni lazima tukae vikao kupanga ratiba ya kumuaga Kamanda Mawazo, Jaji ametoa maelekezo kwamba viongozi wa CHADEMA, familia ya marehemu na Jeshi la Polisi wakae pamoja kupanga ratiba kamili.”
“Tutaheshimu maelekezo ya Jaji lakini hatutakubali kuonewa, muwe na imani kwamba haki itatendeka… tunakwenda kwenye vikao lakini tunahitaji kumaliza jambo hili kuanzia kesho, tutamuaga Mawazo kwa heshima anayostahili katika eneo ambalo tutawatangazia.” >>> Freeman Mbowe.
Hii hapa sauti ya Freeman Mbowe nje ya Mahamaka Kuu Mwanza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE