Klabu ya Real Madrid imeendelea kushika usukani kwa miaka 11 sasa katika kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kupitia mapato yake…kwa msimu wa 2014/15 imeingiza kiasi cha Euro milioni 577.
Real Madrid inafatiwa na mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na euro milioni 560.8, huku Man United wakiwa nafasi ya tatu kwa kujipatia euro milioni 519.5.
Kampuni ya Deloitte inayotayarisha mapato ya klabu hizo imesema kuna uwezekano mkubwa Man United wakawapita Real Madrid wakati wa kutolewa kwa orodha ijayo baada ya miezi 12.
Manchester United walishuka kutoka nafasi ya pili hadi ya tatu baada ya kushuka kwa mapato yao lakini Deloitte wamesema ukuaji wa kibiashara na uwezo wa kupata mikataba mikubwa kama Adidas kila mwaka, vimesaidia sana klabu hiyo.
Kutokana na mkataba mpya wa haki za utangazaji katika runinga wa thamani ya £5.1bn utakaoanza msimu wa 2016-17, Real Madrid huenda ikatatizika kupata mapato ya juu.
Hii ndio Orodha kamili mtu wangu
Nafasi mwaka huu (mwaka jana) | Klabu | Mapato ya 2014/15 (euro m) (Mapato ya 2013/14) | Mapato ya 2014/15 (£m) (Mapato ya 2013/14) |
1. | Real Madrid | 577 (549.5) | 439 (459.5) |
2. | FC Barcelona | 560.8 (484.8) | 426.6 (405.4) |
3. | Manchester United | 519.5 (518) | 395.2 (433.2) |
4. | Paris Saint-Germain | 480.8 (471.3) | 365.8 (394.1) |
5. | Bayern Munich | 474 (487.5) | 360.6 (407.7) |
6. | Manchester City | 463.5 (416.5) | 352.6 (348.3) |
7. | Arsenal | 435.5 (359.3) | 331.3 (300.5) |
8. | Chelsea | 420 (387.9) | 319.5 (324.4) |
9. | Liverpool | 391.8 (305.9) | 298.1 (255.8) |
10. | Juventus | 323.9 (279) | 246.4 (233.3) |
11. | Borussia Dortmund | 280.6 (261.5) | 213.5 (218.7) |
12. | Tottenham Hotspur | 257.5 (215.5) | 195.9 (180.2) |
13. | Schalke 04 | 219.7 (214) | 167.1 (179) |
14. | AC Milan | 199.1 (249.7) | 151.5 (208.8) |
15. | Atletico de Madrid | 187.1 (169.9) | 142.3 (142.1) |
16. | AS Roma | 180.4 (127.4) | 137.2 (106.5) |
17. | Newcastle United | 169.3 (155.1) | 128.8 (129.7) |
18. | Everton | 165.1 (144.1) | 125.6 (120.5) |
19. | Internazionale | 164.8 (162.8) | 125.4 (136.1) |
20 (New) | West Ham United | 160.9 (139.3) | 122.4 (116.5) |
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE