Moja kati ya vyakula vinavyomletea mlaji wake harufu kali ni vitunguu swaumu ambavyo huumika kama viungo kwenye chakula.
Vitunguu swaumu vina vitu fulani ndani yake ambavyo hujitokeza pale kinapokatwa, kusagwa au hata kutafunwa vitu hivi kitaalamu hufahamika kama Allicin na Allin na hivi ndio hasa husababisha harufu kali ambayo hutokea baada ya mtu kula vitunguu swaumu au vyakula vilivyoungwa kutumia vitunguu swaumu.
Pamoja na hayo vitunguu swaumu vina faida kubwa sana mwili mwa mwanadamu na faida hizo huletwa na hii Illin ambayo inatajwa kuwa sababu ya harufu yake mbaya na moja kati ya faida zake ni jinsi ambavyo vitunguu swaumu husaidia kupambana na bacteria wanaoleta magonnjwa mbalimbali na virusi tofauti.
Mbegu ya Binzari
Mbegu ya Binzari hutumika kwenye mapishi ambapo huleta ladha nzuri kwenye chakula, hata hivyo mbegu hizi husababisha harufu mbaya ambayo inabakia mdomoni kwa muda mrefu, kama unataka kupunguza harufu mbaya unaweza kuipunguza kwa kunywa maji mengi na kutumia vyakula vingine ambavyo vinatumika kupunguza harufu ambavyo havina harufu kali.
Nyama Nyekundu.
Nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula vinavyosababisha harufu mbaya mdomoni na tumboni, ni vigumu kwa watu wengi kukubaliana na hili kwa kuwa nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula vinavyopendwa sana na watu.
Tafiti zinaonyesha kuwa jasho jingi ambalo husababishwa na mafuta yanayoganda mwilini kutokana na ulaji wa nyama nyekundu ni moja kati ya vitu ambavyo huleta harufu mbaya kwenye mwili wa mwanadamu.
Kama unataka kupunguza harufu kutokana na nyama nyekundu ni vyema ukapunguza na kuanza kula nyama itokanayo na samaki na wanyama wengine wa baharini .
Mboga Za Majani
Baadhi ya mboga za majani zinasababisha harufu mbaya mwilini nazo ni cauliflower, kabichi, broccoli na nyinginezo.
Tunashauriwa kula mboga za majani kwa wingi kwa sababu hazina mafuta na zinaongeza vitamin mwilini lakini zina madini aina ya sulphur ndani yake ambayo husababisha harufu mbaya.
Kahawa
Kahawa nayo iko kwenye orodha ya vyakula ambavyo vinasababisha harufu mbaya mdomoni na mwilini kwa jumla, moja vitu ambavyo vimo ndani ya kahawa ambavyo ni Caffeine husisimua mfumo wa mishipa ya fahamu mwilini na husababisha mtu avuje jasho kwa wingi kuliko kawaida.
Pia ile acid ambayo iko ndani ya kahawa hufanya mate yakauke mdomoni na hapo bacteria na vijidudu vingine vyenye kufanya harufu mbaya iwepo mdomoni hujitokeza kwa wingi, kutafuna Big G huweza kusaidia kutatua tatizo hili, tafuna Big G mara tu baada ya kunywa kahawa na hapo utazuia harufu mbaya mdomoni.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook