Shirika la Fox linalomiliki chombo cha habari ya Fox News hapa Marekani Jumanne limekubali kulipa fidia ya dola milioni 787.5 kutokana na mashitaka ya kuharibiwa jina yaliyowasilishwa na kampuni ya kusimamia uchaguzi ya Dominion Voting Systems.
Mwanzoni kampuni ya Dominion ilikuwa imedai fidia ya dola bilioni 1.6 za kimarekani kutokana na kesi hiyo iliyowasilishwa 2021, wakati ikiongozwa na jaji wa mahakama ya juu Eric Davis mjini Willmington kwenye jimbo la Delaware.
Shirika la Fox linalomiliki chombo cha habari ya Fox News hapa Marekani Jumanne limekubali kulipa fidia ya dola milioni 787.5 kutokana na mashitaka ya kuharibiwa jina yaliyowasilishwa na kampuni ya kusimamia uchaguzi ya Dominion Voting Systems.
Hatua hiyo imepelekea kujiepusha na kesi ambayo ingeliletea shirika hilo kubwa la habari matatizo makubwa ya kisheria ,kutokana na madai ya uongo kwamba uchaguzi mkuu wa 2020 hapa Marekani uliibwa.
Hatua hiyo ilitangazwa na Fox, Dominion pamoja na jaji aliyekuwa akiiongoza kesi hiyo, mbele ya jopo la watu 12 lililochaguliwa Jumanne asubuhi, wakati kesi yenyewe ikitarajiwa kuanza baadaye saa za adhuhuri.
Mkurugenzi mkuu wa Dominion John Poulos wakati akitangaza fidia waliyopewa alisema kwamba Fox ilikiri kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni yake.