Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group ‘CMG’ Ruge Mutahaba leo August 25, 2017 amezungumzia mambo mbalimbali hasa kusuhusu uchumi wa nchi na namna Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira mazuri ya fursa kwa Watanzania.
Pamoja na mengine haya hapa mambo 10 makubwa Ruge Mutahaba ameyazungumzia.
RUGE: Naamini Tanzania ina fursa nyingi sana. Tanzania ni nchi masikini sana. Nchi masikini, yenye matatizo ndiyo nchi bora kwa fursa.
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Basi kama hii nchi ndiyo masikini, basi ndiyo nchi bora kwa fursa lazima iwe na fursa nyingi zaidi za kufanikiwa na kufanya vitu vingi
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Tumegundua changamoto kubwa kuliko zote, sio ya fursa hadi nchi, ni hatuzungumzii soko linataka nini. Wengi hawajui soko linataka nini
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Soko ndio linatengeneza mahitaji nasi tubadilike. Tujiulize miaka mitano iliyopita ziliuzwa simu kutoka South, nani sasa anaagiza?
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Soko ni kichwani sio sehemu. Hakuna sehemu unapoweza kuita soko, soko ni mwisho. Mtu wa mwisho ndiye anatengeneza soko.
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Ndiyo maana kuna mnyororo wa thamani, mmoja anaweza kutengeneza simu na mwingine akatengeneza cover ya simu.
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Nilizungumza na Serikali ina kazi, wananchi wanaelewaje hivi vitu? Inabidi tufanye kazi kubwa kukuza na kuwafanya waelewe ugunduzi.
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Sisemi kwa ubaya na nisieleweke vibaya, viongozi wetu hawatengenezi msisimko wa kiuchumi, hawatengenezi mazingira ya kukuza uchumi.
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Hawatengenezi mazingira ya kufanya watu wajue soko linataka nini na wao watengeneze nini ili tuwe tunasambaza zaidi.
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
RUGE: Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanafanya kazi nzuri lakini wameweka nguvu kwenye mambo ya kijamii kutatua matatizo kuliko kubuni mbinu mpya.
— AyoTV (@ayotv_) August 25, 2017
Mtambo uliowashwa na Ruge Mutahaba kwenye Clouds 360