Twaweza leo August 30, 2017 imetoa ripoti ya matokeo ya utafiti mpya kuhusiana na masuala ya huduma za afya ambayo inaonesha kuwa 70% ya wananchi wanaokwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya hawapati dawa na vifaa tiba vya kutosha changamoto ambayo imeongezeka kutoka 62% mwaka 2015.
Katika utafiti huo imeonekana kuwa 76% ya wananchi ambao wanahudhuria katika vituo vya afya vya serikali hupata huduma ndani ya saa moja huku upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ikionekana kuwa changamoto.
VIDEO: Mambo matatu Zitto kayasema kuhusu utafiti wa TWAWEZA leo
VIDEO: Ya kufahamu kwenye taarifa ya Haki za Binadamu na Biashara mwaka 2016