Ipo mitazamo tofauti juu ya wanaume wanaofuga ndevu, wapo wanaosema mwanaume kufuga ndevu humwongezea mvuto, wengine wakisema ni dalili ya uchafu na kutojipenda na mengine neyo mengi tu husemwa.
Hata hivyo baada ya kukutana na mijadala mbalimbali kuhusu suala hili kwenye mitandao ya kijamii, Ayo TV na millardayo.com ilitafuta mtazamo wa kitaalamu ili kujua jambo hili.
Shirika la Utangazaji la BBC lilishawahi kuandika katika chapisho la Maambukizi ya Hospitalini, ulifanywa utafiti ambapo wanaume 408 wenye ndevu na wasio na ndevu walitumiwa kwa kufanya uchuguzi huo.
Wanaume wote walipitishiwa kifaa maalumu kwenye videvu vyao ili kuona kama kuna vimelea vyovyote vinavyopatikana kwenye videvu na madhumuni makuu ya kufanya hivyo ni kwamba wataalamu wanaeleza kwamba hospitalini ndipo sehemu ambapo kuna maambukizi mengi sana ya vimelea mbalimbali.
Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa wanaume ambao hawakuwa na ndevu walikuwa hatarini kwa mara tatu zaidi wanabeba na kutunza vimelea hivyo kwenye ngozi zao za kidevu tofauti na wanaume ambao walikuwa wana ndevu.
Utafiti huu ukisapotiwa na tafiti nyingine ulihitimisha kuwa kunyoa ndevu mara nyingi husababisha kuchubuka kwa ngozi na hivyo kutengeneza makazi ya bakteria na mazalia yao.
BABA DIAMOND – “SIJAWAHI KUONGEA NA ZARI, WEMA NA HAMISA NIMEONGEA NAO”