Manchester Evening News inasema Man United wanataka kuwasajili mabeki wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong na Edmond Tapsoba.
Wawili hao wameisaidia Leverkusen kileleni mwa Ligi ya Ujerumani Bundesliga msimu huu, huku wakiwa ndio timu pekee ambayo haijafungwa katika ligi tano bora za Ulaya.
Frimpong, 23, anaweza kuchukua nafasi ya Aaron Wan-Bissaka katika nafasi ya beki wa kulia, wakati Tapsoba mwenye umri wa miaka 25 atakuwa chaguo kuchukua nafasi ya Jonny Evans, Raphael Varane, Harry Maguire na Victor Lindelof katika safu ya ulinzi ya kati.