Mchezo wa mwisho wa Kundi F wa Europa League kati ya timu ya Sassuolo ya Italia ambayo ilikuwa icheze dhidi ya KCR Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, mchezo umeahirishwa hadi Ijumaa ya December 9 Saa 14:30 mchana kutokana na hali ya hewa.
Mchezo huo ambao Mbwana Samatta kapangwa kuanza, umeahirishwa kwa sababu ya ukungu uliosababisha watu wasionane uwanjani, ikumbukwe kuwa KRC Genk anacheza mchezo huu kukamilisha ratiba lakini tayari ameshafuzu hatua inayofuata.
Hali ya hewa ilivyo ktk uwanja wa Mapei ambao mchezo wa EuropaLeague Sassuolo vs KRC Genk unatakiwa kuchezwa, hadi sasa mchezo haujaanza. pic.twitter.com/NZPhbFxqCV
— millard ayo (@millardayo) December 8, 2016
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0