Waziri wa mambo ya ndani Mh Mwigulu Nchemba August 9, 2016 alifanya ziara kwenye kambi za wakimbizi za Katumba na Mishamo zilizopo mkoani Katavi.
Baada ya kumaliza ziara hiyo Waziri huyo aliyaongea haya>>>>nimefanya ukaguzi kwenye kambi ya wakimbizi ya KATUMBA ambako kuna zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea kwa majirani zetu Burundi na baadae tuliamua kuwapa uraia wa Tanzania mwaka 2009′- Mwigulu
‘Zoezi hili la uhakiki linafanyika ilikuchunguza mienendo yao na uwepo wao kwenye eneo la kambi.Kumekuwepo nataarifa za baadhi ya ndugu zetu hawa kujihusisha na watu waovu,kufanya vitendo vya kibaguzi na kutoka nje ya kambi zao na kwenda nchi jirani bila kibali- Mwigulu
‘Nimewaagiza vyombo vya usalama na kupitia serikali za mitaa kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, Tanzania hatua tabia za kibaguzi,moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru’- Mwigulu
‘Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi,kuishi na kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na vyakibaguzi.Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani yetu’- Mwigulu
Msikilize zaidi Mwigulu Nchemba kwa kubonyeza play hapa chini.
ULIIKOSA HII YA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA KUHUSU RAIA WA CHINA KUFANYA UNYANYASA KWA WATANZANIA BASI ISIKILIZE HII SAUTI HAPA